Swahili
Sorah Abasa ( He frowned )

Verses Number 42

عَبَسَ وَتَوَلَّىSorah Abasa ( He frowned ) Verse Number 1
Alikunja kipaji na akageuka,
أَن جَاءَهُ الأَعْمَىSorah Abasa ( He frowned ) Verse Number 2
Kwa sababu alimjia kipofu!
وَمَا يُدْرِيكَ لَعَلَّهُ يَزَّكَّىSorah Abasa ( He frowned ) Verse Number 3
Na nini kitakujuulisha pengine yeye atatakasika?
أَوْ يَذَّكَّرُ فَتَنفَعَهُ الذِّكْرَىSorah Abasa ( He frowned ) Verse Number 4
Au atawaidhika, na mawaidha yamfae?
أَمَّا مَنِ اسْتَغْنَىSorah Abasa ( He frowned ) Verse Number 5
Ama ajionaye hana haja,
فَأَنتَ لَهُ تَصَدَّىSorah Abasa ( He frowned ) Verse Number 6
Wewe ndio unamshughulikia?
وَمَا عَلَيْكَ أَلاَّ يَزَّكَّىSorah Abasa ( He frowned ) Verse Number 7
Na si juu yako kama hakutakasika.
وَأَمَّا مَن جَاءَكَ يَسْعَىSorah Abasa ( He frowned ) Verse Number 8
Ama anaye kujia kwa juhudi,
وَهُوَ يَخْشَىSorah Abasa ( He frowned ) Verse Number 9
Naye anaogopa,
فَأَنتَ عَنْهُ تَلَهَّىSorah Abasa ( He frowned ) Verse Number 10
Ndio wewe unampuuza?
كَلاَّ إِنَّهَا تَذْكِرَةٌSorah Abasa ( He frowned ) Verse Number 11
Sivyo hivyo! Huku ni kukumbushana.
فَمَن شَاء ذَكَرَهُSorah Abasa ( He frowned ) Verse Number 12
Basi anaye penda akumbuke.
فِي صُحُفٍ مُّكَرَّمَةٍSorah Abasa ( He frowned ) Verse Number 13
Yamo katika kurasa zilizo hishimiwa,
مَّرْفُوعَةٍ مُّطَهَّرَةٍSorah Abasa ( He frowned ) Verse Number 14
Zilizo inuliwa, zilizo takaswa.
بِأَيْدِي سَفَرَةٍSorah Abasa ( He frowned ) Verse Number 15
Zimo mikononi mwa Malaika waandishi,
كِرَامٍ بَرَرَةٍSorah Abasa ( He frowned ) Verse Number 16
Watukufu, wema.
قُتِلَ الإِنسَانُ مَا أَكْفَرَهُSorah Abasa ( He frowned ) Verse Number 17
Ameangamia mwanaadamu! Nini kinacho mkufurisha?
مِنْ أَيِّ شَيْءٍ خَلَقَهُSorah Abasa ( He frowned ) Verse Number 18
Kwa kitu gani amemuumba?
مِن نُّطْفَةٍ خَلَقَهُ فَقَدَّرَهُSorah Abasa ( He frowned ) Verse Number 19
Kwa tone la manii, akamuumba na akamkadiria.
ثُمَّ السَّبِيلَ يَسَّرَهُSorah Abasa ( He frowned ) Verse Number 20
Kisha akamsahilishia njia.
ثُمَّ أَمَاتَهُ فَأَقْبَرَهُSorah Abasa ( He frowned ) Verse Number 21
Kisha akamfisha, akamtia kaburini.
ثُمَّ إِذَا شَاء أَنشَرَهُSorah Abasa ( He frowned ) Verse Number 22
Kisha apendapo atamfufua.
كَلاَّ لَمَّا يَقْضِ مَا أَمَرَهُSorah Abasa ( He frowned ) Verse Number 23
La! Hajamaliza aliyo muamuru.
فَلْيَنظُرِ الإِنسَانُ إِلَى طَعَامِهِSorah Abasa ( He frowned ) Verse Number 24
Hebu mtu na atazame chakula chake.
أَنَّا صَبَبْنَا الْمَاء صَبًّاSorah Abasa ( He frowned ) Verse Number 25
Hakika Sisi tumemimina maji kwa nguvu,
ثُمَّ شَقَقْنَا الأَرْضَ شَقًّاSorah Abasa ( He frowned ) Verse Number 26
Tena tukaipasua pasua ardhi kwa nguvu,
فَأَنبَتْنَا فِيهَا حَبًّاSorah Abasa ( He frowned ) Verse Number 27
Kisha tukaotesha humo nafaka,
وَعِنَبًا وَقَضْبًاSorah Abasa ( He frowned ) Verse Number 28
Na zabibu, na mimea ya majani,
وَزَيْتُونًا وَنَخْلاSorah Abasa ( He frowned ) Verse Number 29
Na mizaituni, na mitende,
وَحَدَائِقَ غُلْبًاSorah Abasa ( He frowned ) Verse Number 30
Na bustani zenye miti iliyo songana baraabara,
وَفَاكِهَةً وَأَبًّاSorah Abasa ( He frowned ) Verse Number 31
Na matunda, na malisho ya wanyama;
مَّتَاعًا لَّكُمْ وَلِأَنْعَامِكُمْSorah Abasa ( He frowned ) Verse Number 32
Kwa manufaa yenu na mifugo yenu.
فَإِذَا جَاءَتِ الصَّاخَّةُSorah Abasa ( He frowned ) Verse Number 33
Basi utakapo kuja ukelele,
يَوْمَ يَفِرُّ الْمَرْءُ مِنْ أَخِيهِSorah Abasa ( He frowned ) Verse Number 34
Siku ambayo mtu atamkimbia nduguye,
وَأُمِّهِ وَأَبِيهِSorah Abasa ( He frowned ) Verse Number 35
Na mamaye na babaye,
وَصَاحِبَتِهِ وَبَنِيهِSorah Abasa ( He frowned ) Verse Number 36
Na mkewe na wanawe -
لِكُلِّ امْرِئٍ مِّنْهُمْ يَوْمَئِذٍ شَأْنٌ يُغْنِيهِSorah Abasa ( He frowned ) Verse Number 37
Kila mtu miongoni mwao siku hiyo atakuwa na lake la kumtosha.
وُجُوهٌ يَوْمَئِذٍ مُّسْفِرَةٌSorah Abasa ( He frowned ) Verse Number 38
Siku hiyo ziko nyuso zitazo nawiri,
ضَاحِكَةٌ مُّسْتَبْشِرَةٌSorah Abasa ( He frowned ) Verse Number 39
Zitacheka, zitachangamka;
وَوُجُوهٌ يَوْمَئِذٍ عَلَيْهَا غَبَرَةٌSorah Abasa ( He frowned ) Verse Number 40
Na nyuso siku hiyo zitakuwa na mavumbi,
تَرْهَقُهَا قَتَرَةٌSorah Abasa ( He frowned ) Verse Number 41
Giza totoro litazifunika,
أُوْلَئِكَ هُمُ الْكَفَرَةُ الْفَجَرَةُSorah Abasa ( He frowned ) Verse Number 42
Hao ndio makafiri watenda maovu.